MWIZI MSANII HATIMAYE ADAKWA

KILA kazi ili ufanikiwe, ni lazima uwe mbunifu, utofautiane na wengine.
Ndivyo ilivyokuwa
kwa mwizi huyu wa kuvunja na kubomoa nyumba, huko Gutu katika Jimbo la Masvingo
nchini Zimbabwe.
Inadaiwa kuwa mwizi
huyo alikuwa akivaa mavazi yanayofanana na mizimu ya Haloween na akijitokeza,
kwa hofu wenye nyumba hukimbia wakiamini wamekutana na mzuka wa kweli.
Huku nyuma, mwizi
huyo huchukua vitu vyote anavyovihitaji na kutoweka. Baada ya muda mrefu,
wakazi hao wakakata shauri na kumwekea mtego uliomnasa kirahisi.

Post a Comment