MIMI NA YUSSUF MANJI TUTAIPELEKA YANGA LEVO ZINGINE AFRIKA

NI wakati wa kicheko kwa
mashabiki wa Dar Young Africans!
Baada ya kunyanyasika kwa
kipindi cha misimu minne huku watani wao wakitakata kwa kutwaa mataji ya Ligi
Kuu na kufanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mambo sasa
yatajipa Jangwani kuanzia msimu ujao.
Hiyo ni baada ya Ghalib Said
Mohammed - GSM kuzungumzia juu ya 'kolabo' yake na Yussuf Manji.
"Kwa sasa mimi siwezi kusema chochote nini nitawafanyia Yanga SC ila ngoja tupate mfumo sahihi wa mabadiliko wa timu yetu ndipo nitawaonesha kwa mara nyingine mapenzi yangu kwa timu hii nini nitawafanyia.
"Najua Yusuph Manji aliifanyia makubwa sana timu hii wakati yeye alivyokuwa hapa kitu ambacho mimi bado sijafikia ila hainikatishi tamaa kuacha kuendelea kuisaida Yanga nitapambana hadi mwisho wa msimu huu kuwa karibu na timu yangu kwa kuwapa ufadhili wote unaohitajika.
"Ujio wa Manji Tanzania umenipa furaha sana na nilishawahi kuongeaga nae awali kabla ya kurudi nchini alinambia nia yake ya dhati kabisa kuja kutaka kuifanya Yanga iwe moja ya timu kubwa barani Afrika baada ya kunipongeza kwa hatua ya mabadiliko tunayoendelea kuyafanyia ya kimuundo wa klabu yetu kwa sasa.
"Imani yangu atakuja tena
Yanga na tutaunganisha nguvu kwa pamoja kuipeleka Yanga kule mashabiki na
wanachama wote wa Yanga wanaopataka kuiona timu yetu inapostahili",

Post a Comment