PANYA 'AFISA' ASTAAFU KUTEGUA MABOMU CAMBODIA


FB_IMG_1622876996965.jpg

PANYA wa Tanzania mwenye sifa ya kufichua mabomu kimataifa amestaafu kazi hiyo nchini Cambodia akijishindia tuzo kwa ushujaa wake katika kazi yake ya kufichua mabomu yaliyotegwa ardhini.

Panya huyo aitwaye Magawa kwa kila ugunduzi alioufanya ulipunguza hatari ya kuumia au kifo kwa watu wa Cambodia.

Katika kazi ya miaka mitano aliyofanya hadi leo Magawa amefanikiwa kugundua mabomu 71 yaliotegwa ardhini pamoja na vilipuzi kadhaa nchini Cambodia na kumfanya kuwa HeroRAT aliyefanikiwa zaidi wa APOPO.

Wasimamizi wake wanasema kwamba panya huyo mwenye umri wa miaka saba ameanza kupunguza kasi yake akielekea kuwa mzee na anahitaji kuheshimu mahitaji yake.

Magawa ni panya mkubwa wa kijeshi wa kiafrika aliyezaliwa nchini Tanzania mnamo Novemba 2014. Alikulia katika kituo cha Mafunzo na Utafiti cha APOPO nchini Tanzania ambapo alijifunza jinsi ya kupata vilipuzi kwa kutumia hisia zake za ajabu za kunusa. Magawa kisha alihamia Siem Reap huko Cambodia mnamo 2016, ambapo alianza kazi yake yenye mafanikio.

No comments