BANANGA ATOFAUTIANA NA LISU KUHUSU DIAMOND

WAKATI Tundu Lissu
akitaka wapenda demokrasia wasimpigie kura za kushinda Tuzo za BET msanii
Diamond Platnums, mwanachama mwenzake wa Chadema, Binamu Bananga, amesema yeye
ni shabiki wa kijana huyo wa Tandale na kwa hiyo atampigia kura.
Katika kushibisha
hoja yake, Bananga amesema pamoja na tofauti za kiitikadi zilizopo baina yao,
linapokuja suala la michezo, muziki na starehe, hivyo ni vitu havina itikadi.
"Mimi ni
shabiki wa Diamond, lazima nitampigia kura, siwezi kuacha kuishabikia Simba kwa
sababu mfadhili wake Mo ni mtu wa CCM. Huwa nachagua vita ya kupigana, vita
ndogo vina gharama kubwa kama hupigani kwa tahadhari.
"Siyo lazima
nile kware wakati nina kuku. Wajibu wangu kisiasa ni mkubwa kuliko kumuombea
mabaya mtanzania anayejiinua, kama humuungi mkono waachie wanaomuunga."

Post a Comment