DUH, GAMBO WA KUHOJI HIFADHI YA BULIGI CHATO?

MIONGONI mwa viongozi vijana waliokuwa vipenzi vya Rais wa Awamu ya Tano, John Pombe Magufuli, ni pamojha na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati ule, Mrisho Gambo ambaye sasa ni Mbunge wa Arusha Mjini.
Lakini kwa namna isiyotarajiwa,
Mbunge huyo ni kama amemgeuka Magufuli, kufuatia kitendo chake cha kuhoji faida
ambayo nchi inapata kwa uwepo wa Hifadhi ya Buligi Chato ambayo ilipandishwa
hadhi kipindi cha JPM.
“Kwenye taarifa ya Waziri anasema hapa kuwa utalii unachangia
pato la taifa kwa asilimia 17 na fedha za kigeni kwa asilimia 25, mimi nadhani
taarifa ya Waziri ni ya zamani sana kwa namna ambavyo janga la corona limeathiri
sekta ya utalii nchini na duniani kote.
“Ukiangali taarifa yake amesema hadi Aprili mwaka 2019 target
ilikuwa kukusanya Tsh bil 584 na sisi tumekusana Tsh bil 89 ambayo ni sawa na
asilimia 15 tu.
“Mchango wa utalii kwa GDP umeshuka kutoka kutoka asilimia
17.5 mpaka asilimia 11.5 na bado wamepandisha tozo za utalii wakati nchi
nyingine za Afrika Mashariki zimeshusha. Dunia nzima inatoa ahuweni kwenye
utalii lakini sisi tunaongeza gharama Mimi naona bado kuna kazi ya kufanya.
“Ninashauri tupitie hifadhi zote za Taifa especially ya
Burigi Chato, mlete hapa mtuambie imepokea wageni wangapi na imeingiza kiasi
gani na inatumia gharama kiasi gani kuendeshwa, sio tunaanzisha hifadhi nyingi
na gharama za uendeshaji zinakuwa kubwa kwa sababu utapeleka watumishi kule
utawalipa, gharama hizi unakuwa mzigo kwa mtalii ndio maana tunapandisha tozo
kila mara.
“jambo jingine, ukienda Kenya, kupima corona ni dola 30 kwa
hospitali za Serikali na dola 50 kwa hospitali private lakini hapa kwetu ni
dola 100, sasa najiuliza kwani corona nayo ni fursa? Kituo cha kupimia corona
(maabara) tuncho kimoja tu. Hili jambo inabidi tuliangalie upya,” amesema
Mrisho Gambo.

Post a Comment