NAHODHA WA SERENGETI BOYS ATUA LIGI KUU SERBIA


Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na nyasi

MOURICE Abraham, aliyekuwa nahodha wa kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17, amejiunga na timu ya Spartak Subotika inayoshiriki Ligi Kuu nchini Serbia.

Kiungo huyo amesaini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo akiwa chini ya usimamizi wa Samaplayer Management na tayari kijana yupo Serbia akisubiri kutambulishwa.

Kampuni hiyo inayomsimamia inaongozwa na nahodha wa timu ya Taifa Stars, Mbwana Samatta kupitia ktk ukurasa wake wa Instagram tayari imeweka moja ya video za mchezaji huyo akiwa katika majukumu yake mapya nchini Serbia.

Licha ya kusajiliwa katika timu ya wakubwa ataanzia kuchezea soka lake katika timu ya vijana chini ya miaka 19 na baadaye ataitumikia timu ya wakubwa.

 

No comments