MAGEREZA WAKANUSHA OLE SABAYA KUGOMA KUOGA

KUKIWA na taarifa kwamba aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya anayeshtakiwa kwa makosa sita ya uhalifu kugoma kuoga mara baada ya kutinga mahabusu gerezani, Mkuu wa Magereza Mkoani Arusha, Godson Mwanagwa amekanusha taarifa hizo.
"Alipokelewa vizuri tu hakuna vurugu zilizotokea, hakuna
tukio kama hilo lililotokea, aliyetoa taarifa mngemuambia amezitoa wapi, Mimi mhusika
nakuambia wanaoripoti ni waongo," alisema Godson Mwanangwa.
Kesi ya Sabaya imekuwa gumzo kubwa
nchini, wananchi kutoka pande zote wakiwa na maoni tofauti. Sabaya atasubiri
mahabusu katika kipindi chote cha kesi yake kwa vile baadhi ya makosa
anayotuhumiwa nayo hayana dhamana.

Post a Comment