DOLA BILIONI 30 KULALA MRADI GESI ASILIA LINDI

WAKATI Serikali ikihaha huku na kule
kuhakikisha Tanzania inakula jasho kutokana na rasilimali zake, Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa amesema Serikali ipo mbioni kuanza kutekeleza mradi wa kimkakati wa
uzalishaji wa gesi asilia ya kimiminika (LNG) mkoani Lindi utakaogharimu dola
za kimarekani bilioni 30.
Amesema kuwa Mradi huo ni moja ya mradi wa kimkakati ambao
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepania
kuutekeleza katika awamu ya sita ambao utakapoanza kutekelezwa itatumika kwa
kipindi cha zaidi ya miaka 25.
Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Juni 5, 2021 wakati wa mkutano
na wadau wa maendeleo wa Wilaya ya Lindi, katika ukumbi wa hoteli ya Sea View
Mjini Lindi.
"Vile viwanja mlivyovichukua anzeni kuvijenga, mradi wa
gesi asilia unakuja, nina amini mradi huu ukianza baada ya kukamilisha
makubaliano, tutafika hatua nzuri."

Post a Comment