KUHUSU CORONA, MSEMAJI WA SERIKALI ASEMA...


Tanzania calls out Kenyan media for false reporting – JamhuriNews.com

 GERSON MSIGWA, msemaji wa Serikali, leo alizungumza na wanahabari, miongoni mwa mambo mengi, alizungumzia ishu ya Covid 19.

"Sasa kwenye eneo hili la ugonjwa wa Corona kumekuwa na maneno mengi na kujazana hofu bila sababu, Rais alichoamua ni kuimarisha juhudi za kupambana na janga hili kwa kutoa nafasi kwanza kwa Wataalamu wetu wakiongozwa na Prof. Said Aboud kufanya tathmini ya kitaalamu na kuishauri Serikali juu ya namna ya kukabiliana na ugonjwa huu.

“Kamati imefanya kazi yake na imewasilisha mapendekezo ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa, jana Rais amekabidhiwa mapendekezo hayo yenye mpango kazi wa kutafuta rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa mpango mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Covid-19 na ya mpango kazi wa uratibu wa utoaji wa chanjo ya ugonjwa huo yaliyowasilishwa na kamati ya wataalamu aliyoiunda kwa ajili ya kuishauri Serikali.
“Sasa haya ni mapendekezo ya Wataalam na Rais ameelekeza mapendekezo haya sasa yaandikiwe andiko na yawasilishwe katika Baraza la Mawaziri ili kujadiliwa na kufanyiwa maamuzi na baada ya hapo Serikali itakuja na tamko juu mapendekezo hayo.”

 

No comments