GRUPU LA WHATSAPP LACHANGIA MIFUKO 300 YA SIMENTI NACHINGWEA BOYS HIGH SCHOOL


IMG_20210605_155846_330.jpg

HAYA ndiyo mambo sasa. Badala ya kutumia magrupu ya whatsApp kwa mambo yasiyo ya msingi, wananchi wa Wilaya ya Nachingwea kupitia grupu lao la Nachingwea yetu, wamejichanga na kununua mifuko 300 ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo.

Baadhi ya wananchi wa Nachingwea ambao wapo ktk kundi sogozi la WhatsApp la NACHINGWEA YETU, wamekabidhi mifuko 300 ya saruji kuunga mkono ujenzi wa mradi mpya wa Nachingwea  Boys High School inayojengwa kwa kutumia mapato ya ndani ya halmashauri ya wilaya ya Nachingwea iliyopo mkoa wa Lindi

Shule hiyo inatarajiwa kukamilika kwake kuchukua wanafunzi 1600 kuanzia kidato Cha Kwanza Hadi Cha sita.

Aidha shule hiyo mpya ya wavulana inatarajiwa kuwa na jumla ya majengo 54 ikiwemo madarasa, mabweni, nyumba za walimu, duka, zahanati na sehemu ya kula chakula.

Shule hiyo inajengwa nje kidogo ya mji wa Nachingwea katika Kijiji cha Chiumbati Kata ya Chiumbati Tarafa ya Naipanga.

Akizungumza wakati wa kupokea mchango huo, aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ambaye kwa sasa ni Katibu Tawala mkoa wa DSM, Hassan Abasi Rugwa, amewashukuru wadau hao wa Nachingwea Yetu Whatsapp group kwa mchango wao na kuwasisitiza wananchi wa Nachingwea kuendelea kushikamana kwa pamoja ili kufanya Mambo makubwa zaidi.

Serikali imeonesha nia ya kuunga mkono ujenzi wa shule hiyo baada ya kuona jitihada za dhati zinazofanywa na wananchi.

No comments