ZIZZOU NA VILLARREAL NCHINI HISPANIA
MWAMBA Zinadine Zidane maarufu kama Zizzou, Mfaransa mwenye asili ya Algeria, anachukuliwa bado kuwa ndiye mchezaji fundi zaidi wa mpira kuwahi kutokea katika soka la kisasa nchini Ufaransa.
Ana kumbukumbu nyingi, lakini ambayo
wengi hawaifahamu ni kwamba kuna 'kauhusiano' flani kati yake na mabingwa wapya
wa Europa League msimu huu, Villarreal.
Akiwa mchezaji wa Real Madrid, mechi
yake ya mwisho kuichezea ilikuwa ni dhidi ya timu hii katika La Liga mwaka
2006.
Na mchezo wake wa mwisho msimu huu,
akiwa kama kocha wa Real Madrid, ulikuwa dhidi ya timu hiyo hiyo, ndani ya Santiago Bernabeu.

Post a Comment