K VANT YAZUA MJADALA MITAANI
WAKATI
kinywaji kikali aina ya K Vant kikiliteka soko la wanywaji wa pombe kali, hali
imegeuka kuwa gumzo mitaani baada ya baadhi kudai 'ukipiga' hayo maji meupe,
kumbukumbu zinapotea.
Kwa
mujibu wa majadiliano hayo, wadau wanasema K Vant ni kinywaji supa sana na kwa
kweli hivi sasa kipo juu kimahitaji sokoni, lakini tatizo lake ni hilo tu;
"Asikuambie
mtu, mimi naipenda sana hii kitu, tatizo lake ni moja tu, kesho nitaamka nikiwa
nimesahau mambo mengi ya jana yake, tofauti na nikinywa pombe zingine kali au
bia," anasema mnywaji mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Zomboko.
Kauli
hiyo imeungwa mkono na watu wengine kadhaa ambao nao wamekiri kuwa licha ya
uzuri wake, wanywaji wake wana tatizo la kupoteza kumbukumbu

Post a Comment