ZARI THE BOSSLADY, DIAMOND PAMOJA ZANZIBAR


IMG_2533.jpg

WAKATI ikifahamika kuwa msanii mkubwa wa muziki wa kizazi kipya nchini, Diamond Platnum kuwa yupo Zanzibar katika harakati za kukamilisha albamu yake, picha zimevuja zikionyesha akiwa pamoja na mzazi mwenzie, Zarina Hassan.

Wawili hao ni wazazi wa watoto wawili, Tiffah na Nilan na uhusiano wao ulishakatika miaka michache iliyopita, kiasi cha kusababisha kukutana kwao Zanzibar kuleta sintofahamu kwa mashabiki wao.

Hata hivyo, baada ya kuachana, bado wanaendelea kuwa na uhusiano wa wazazi, kwani mara kadhaa wamekuwa wakitembeleana.

No comments