TANZANIA, BRAZIL KUSHIRIKIANA KIMICHEZO


Azam TV - UTEUZI: Rais John Magufuli pia amemteua Innocent Bashungwa kuwa  Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, wizara ambayo awali ilikuwa  ikiongozwa na Dkt. Harrison Mwakyembe. Waziri Bashungwa katika kipindi cha

 WAKATI ikifahamika kuwa taifa la Brazil ni mahiri katika soka duniani, jambo la kufurahisha ni kuwa nchi hiyo sasa imekubali kushirikiana na Tanzania ili kuangalia namna ya kufanya programu ya kubadilishana wakufunzi.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesema Nchi ya Brazil ipo tayari kushirikiana kitaalamu na Tanzania kati Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichopo Jijini Mwanza kwa kufanya Programu ya kubadilishana Wakufunzi wa michezo.

Bashungwa alisema jana Mei 21, 2021Jijini Dar es Salaam alipokutana na Balozi wa nchi hiyo Antonio Augusto Martins Cesar ambapo amemuomba  kuialika timu ya Taifa ya Wanawake ya nchi hiyo kuja kucheza na Tanzania ili kuleta motisha ya kukuza Michezo ya wanawake ikiwa ni sehemu ya kutimiza maagizo aliyoyatoa Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.

Naye Balozi huyo amemshukuru Waziri Bashungwa kwa kupata muda wa kuonana nae ambapo amepokea maombi ya ushirikiano baina ya Brazil na Tanzania Katika sekta ya Michezo na kuahidi kuwasiliana na serikali yake mapema iwezekanavyo ili kujua ni jinsi gani wanaweza kufanya mabadilishano ya wakufunzi wa michezo na pia kukaa na Idara ya Michezo kuainisha ni namna gani wanaweza kukisaidia Chuo cha Maendeleo ya Michezo Nchini. Aidha , Balozi huyo ameridhia kuialika timu ya Taifa ya Wanawake ya nakuahidi kulifayia kazi suala hilo.

No comments