WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMA NYONGO SOKONI KARIAKOO
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu leo alitembelea soko Kuu la Kariakoo na kuzungumza na wafanyabiashara. Hii hapa ripoti yake kwa wananchi kupitia mtandao wake wa kijamii.
"Jana tar 22/5/2021 nilifanya ziara Sokoni Kariakoo kufuatilia
jumbe nyingi za simu nilizopokea kutoka kwa wafanyabiashara wa Soko hili. Baada
ya kuwasikiliza wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo nakiri pasi na shaka kuwa
lipo tatizo ambalo tunapaswa kulitatua haraka ili kurudisha Hadhi na Heshma ya
Soko la Kariakoo.
"Tuhuma na kero za wafanyabiashara nilizopokea ni pamoja
na mfanyabiashara kudaiwa rushwa ya hadi shilingi milioni 4 ili aweze
kukodishwa kizimba/kigoli, kodi kubwa ya shilingi laki 7 kwa mwezi kwa
wapangaji wa vigoli vya nje ya soko halafu mbele kuna mpangaji tena anaeuza
bidhaa hizohizo akilipa kodi ya shilingi 51,000 kwa mwezi.
"Uwepo wa tozo kubwa kwa
wafanyabiadhara wa meza, kutoruhusiwa magari ya karoti na mbogamboa kushusha
mizigo sokoni Kariakoo kama ilivyokuwa zamani, uwepo wa madalali wa vigoli
pamoja na uwepo wa ubadhilifu wa fedha za mali za Shirika la Masoko ya Kariakoo.
"Ili kutatua kero hizi, nimeamua kuunda Kamati huru ya
kuchunguza tuhuma hizi na kuniletea Taarifa ndani ya siku 14.
"Nitoe rai kwa wafanyabiashara wa sokoni Kariakoo
kuendelea kuwa watulivu na kufanya biashara zao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni
na Taratibu. #KaziIendelee

Post a Comment