DAVIDO ASOGEZA MCHUMA WA BILIONI MOJA BANDANI

MSANII nyota kutoka Nigeria, Davido amenunua gari aina ya Rolls Royce yenye thamani ya dola za Marekani 450,000 ambazo kwa pesa za madafu ni zaidi ya bilioni moja.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, nyota huyo amesema baada ya kula bata kwa kipindi kirefu na kutoa misaada mingi kwa wahitaji, ameamua kujizawadia.
Akiwa Marekani, Davido ameandika baada ya kukabidhiwa mchuma
huo wa kifahar "Tunafanikiwa kwa kusaidia wengine lakini usiache kujizawadia,
MUNGU Ni Mwema Nimejipatia Rolls Royce yangu ya kwanza"

Post a Comment