ROMA MKATOLIKI AKOSA USHAWISHI KWA DEMU WAKE KUHUSU SIMBA KUTOLEWA CAF CHAMPIONS LEAGUE


AUDIO | Roma Mkatoliki Diss Track (TunaishiNao Remix) - MONI CENTRALZONE |  Download - DJ Mwanga

MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Fleva, Roma Mkatoliki, amekiri kwamba ni ngumu sana kumfahamisha mwanamke wake kuwa timu anayoishabikia ya Simba, imeshinda, lakini imetolewa katika mashindano.

Kwenye akaunti yake kunako mitandao ya kijamii, Roma Mkatoliki ameandika: Hamna kazi ngumu kama kumuelewesha demu kuwa tumeshinda aafu tumetolewa.

Hapa alikua anamaanisha licha ya ushindi mzuri wa Simba wa mabao 3-0  dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, Simba haikufuzu hatua ya nusu fainali kwani katika mchezo wa kwanza kule Johannesburg, wekundu hao wa Msimbazi, walipigwa 4-0.  

No comments