WAZIRI AMTEMBELEA KING KIKI KUMJULIA HALI
WAZIRI wa Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa jana alimtembelea nyumbani kwake mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi, Kikumbi Mwanza Mpango maarufu kama King Kiki ambaye ni mgonjwa.
Katika salamu zake kwa mwanamuziki
huyo aliyetamba na kibao chake cha Kitambaa Cheupe nyumbani kwake Temeke jijini
Dar es Salaam, Waziri aliwataka wasanii nchini kuhakikisha wanamiliki Bima za
Afya ambazo zitawasaidia wanapokua wagonjwa wakati wowote.
"Wizara itaendelea kufuatilia kwa ukaribu matibabu yako
na kwa sababu daktari wako tuna mawasiliano ya karibu tutakuwa tunajua hali
yako inavyoendelea kila siku," alisisitiza Waziri Bashungwa.
Kwa upande wake, King Kikii alimshukuru Waziri Bashungwa kwa
kumtembelea na kumfariji pia amemuomba Waziri amfikishie Salam zake kwa Rais Samia
Suluhu Hassan na kumpongeza kwa kazi nzuri ya kuliongoza Taifa.
Mzee King Kikii ametumia nafasi hiyo kuwaasa wanamziki na
wasanii wengine kuwa na nidhamu katika kazi ili kuendelea kufanya sanaa kwa
muda mrefu.

Post a Comment