WATATU WADAKWA WAKIJIFANYA WAZEE WA KITENGO

VIJANA watatu, wakitambua kwamba wafanyakazi wa Idara ya Usalama wa Taifa (Tiss) ni watu wanaoogopwa katika jamii, wamejitwika utumishi hewa wa idara hiyo na kujaribu kutapeli watu mkoani Shinganya.
Lakini Jeshi la Polisi baada ya
kudokezwa na wasamaria wema, wamewakamata vijana hao na baada ya kupekuliwa, wamekutwa
na vitambulisho vya Tiss, vitambulisho viwili vya JWTZ, Mhuri na barua zenye
nembo ya Jeshi la Polisi.
Waliokamatwa ni Dismond Zakaria ambaye ni Mwalimu (33), Feisal Husein Mtaalamu wa Teknolojia ya Mawasiliano (27) na Mfanyabiashara Juma Almasi (35).
Kamanda wa Polisi, (ACP) Debora Magiligimba, amesema
watuhumiwa hao wamekamatwa Mei 26, 2021 katika msako maalumu wa kupambana na wahalifu.

Post a Comment