MKUU WA MKOA ATAKA WATU WAKE KUPOMBEKA


imgonline-com-ua-twotoone-Y3CdGG4GrNxs.jpg

KATIKA kile anachoamini kuwa kwa kufanya hivyo kutaongeza kiwango cha kodi serikalini, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila, amewataka wakazi wa mkoa huo kunywa pombe kwa wingi.


Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na uongozi wa TRA.


Alisema watu wakiacha kunywa pombe maana yake mapato ya serikali yatapungua kwa sababu unywaji pombe unaongeza kodi za serikali.

Kuhusu baadhi ya kero za baa kupiga kelele za muziki, Chalamila alisema hapo ndiyo mahala pake, kwa kuwa asingetegemea sehemu kama hizo ziwe na utulivu.

Aidha, alitaka TRA kukusanya mapato ya serikali kwa “kuwafinya kidogo” wafanyabiashara wasiotaka kulipa kwa hiari.


No comments