WASANII WAIJIA JUU BASATA
SIKU chache baada
ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), kutoa mwongozo kwa wasanii wa muziki wa
kizazi kipya kupeleka kazi zao ili kuhakikiwa kabla ya kuziruhusu kupigwa
redioni na katika televisheni, wasanii wameibuka na kuipinga kila kona.
Lengo la Basata
katika mwongozo huo, ni kile ilichosema kulinda maadili ya maudhui na hata
uonekanaji kwenye video.
Wasanii hao
wamesema jambo hilo ni la kizamani na linalolenga kurudisha nyuma sanaa hiyo
ambayo sasa imekua kubwa na yenye kutoa ajira za kutosha kwa maelfu ya vijana
nchini.
Waliopinga waziwazi
ni pamoja na mkongwe wa Bongo Fleva, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA
ambaye pia ni Mbunge wa Muheza kupitia CCM.
Mwana FA ameitaka
Basata kufikiria upya kuhusu jambo hilo, kwani linaenda kuiumiza sanaa. Nyota mwingine
wa muziki huo wa kizazi kipya, Ney wa Mitego, ambaye amekwenda mbali zaidi na
kudai anafanya mchakato wa kujitoa katika Baraza hilo ili awe huru wa kuweza
kufanya muziki na kusambaza mwenyewe mitaani.
Z Anto pia ni
miongoni mwa wasanii wanaolalamikia hatua hiyo ya Basata, akidai kitendo hicho
kinakwenda kuua mitaji ya wasanii, kwani kazi hizo zinakwenda kuhakikiwa ikiwa
tayari wameshgrekodi au kutengeneza video.

Post a Comment