WALIOPITA HAPA HAWAKURUDI KUSIMULIA

KWA kawaida,
binadamu tunafanya mambo mengi katika maisha yetu kabla ya kufa. Baadhi ya
tunayofanya, hutupa burudani na mafunzo pia kwa wenzetu.
Mathalan, yapo
mambo ambayo tunapoyapitia, tunapata pia muda wa kuwasimulia wengine ili nao
wafurahi, waguswe au hata wajiandae kukabiliana nayo pindi yakiwakuta.
Lakini kwa Kisiwa
cha Goree, kilichopo katika jiji la Dakar, kule nchini Senegal ni tofauti kwa
miaka ile mingi iliyopita.
Wakati ule mchafu
wa biashara ya watumwa, katika kisiwa hicho, kulikuwa na jengo maalum la
kusubiria abiria wakati meli, mashua, au boti zikitia nanga. Wazungu
walilijenga jengo hilo na kuuweka mlango ambao ulipata umaarufu mkubwa kwa jina
la A Door Of No Return wakimaanisha, ukipita katika mlango huo, hautarudi tena
ulikotoka.
Mamia kwa maelfu ya
watumwa kutoka nchi za Afrika Magharibi walipitia mlango huu na kupelekwa Ulaya
na Marekani kwenda kufanya kazi katika mashamba na viwandani. Wengi pia
walioumwa au kuleta ubishi, walitoswa baharini na kufa.
Rais Barak Obama wa
Marekani wakati wa ziara yake barani Afrika, alifika katika nchi hiyo na
kutembelea lango hilo. Aliposimuliwa kilichotokea, alitoa machozi kwa uchungu.

Post a Comment