BARAKOA: VAZI RASMI IKULU, MITAANI HAWALIJUI


Hatua ya rais Samia kuhimiza uvaaji barakoa wazusha gumzo | Matukio ya  Afrika | DW | 11.05.2021

WAKATI Rais Samia Suluhu Hassan akionyesha kwa vitendo juu ya hofu yake kwa ugonjwa wa Covid 19, Watanzania wengi bado hawaamini kama nchi yao siyo kisiwa, hivyo wanaendelea kujiachia bila tahadhari juu ya janga hilo la kidunia.

Shughuli zote za kiserikali hivi sasa zinaendana na vazi la barakoa, linalozuia maambukizi ya ugonjwa huo, lakini mitaani ni kama vile watu hawajui lolote juu ya Covid 19 kwani, kuvaa barakoa ni gharama isiyo na sababu.

Ndani ya mabasi ya abiria maarufu kama daladala, watu wanaendelea kujazana bila tahadhari yoyote kuchukuliwa, katika maeneo ya soko, stendi, misibani, harusi na kote huko, mambo ni kama kawaida, kuvaa barakoa ni kupenda mwenyewe.

Kama serikali imetambua uwepo wa ugonjwa huu, ni budi kuchukua hatua za makusudi, kulazimisha taifa zima kutambua janga hili. Daladala ziwe levo siti, maji tiririka yawepo kila sehemu na umbali kati ya mtu na mtu katika shughuli za kijamii izingatiwe. 

No comments