TRA YAITIKIA WITO WA MAMA SAMIA


Shouldn't Mama Samia stress gender equality? - The Citizen

 WIKI chache tu baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutaka serikali kutotumia nguvu katika kudai kodi kwa wafanyabiashara, Mamlaka ya Mapato Nchini TRA, leo imetangaza kuzifungulia akaunti zote za wafanyabiashara zilizokuwa zimefungwa kwa kudaiwa kodi.

Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa TRA, Richard Kayombo, alitoa msimamo huo mbele ya wahariri wa vyombo vya habari wakati akitoa mada kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri TEF mjini Morogoro leo.

"Si kawaida kushikilia akaunti ya mfanyabiashara na uamuzi huu mara nyingi unakuwaga wa mwisho kabisa baada ya jitihada zingine kushindikana ikiwemo majadiliano na mhusika," amesema Kayombo.

"Tumeamua kuziachia hizi akaunti ili sasa tuwe tunakaa mezani na kujadiliana na wafanyabiashara wenye madeni namna bora ya kulipa taratibu taratibu na tunaachana na ule wa kushikilia akaunti zao," alisema.

 

No comments