WAKATI AKIZUSHIWA UGONJWA, JK ALA BATA ZANZIBAR


Samuel Eto'o Akutana na Kikwete Masaki, Dar - Global Publishers

MAPEMA siku mbili hizi, kumeenea uvumi kwamba Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete ni mgonjwa.

Leo, mwanaye wa kiume, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete aliondoa ukimya na kusema, baba yake ni mzima wa afya nyingi akiendelea na majukumu yake ya kila siku.

Sasa, taarifa mpya zimekuja kwamba kiongozi huyo wa zamani wa Tanzania, mwingi wa tabasamu usoni, alikuwepo Zanzibar, huko Nungwi, akila bata katika hoteli ya Kodoti Villas.

Inadaiwa, mzee wa Msoga alikuwepo hotelini hapo kwa wiki nzima akiwa anaendelea na mchakato wa kuandika kitabu chake.

Pia, inasemekana jana, May 27 mwaka huu, alikuwepo Chuo Kikuu saa sita vmchana akiwatunuku shahada mbalimbali wanafunzi wa Chuo Kikuu katika mahafali ya 51 duru ya 1. 

 

No comments