MUME AMUUA MKEWE AKIHISI ANAMLOGA

DUNIA haina jema. Katika umri wao wa uzeeni, mume mwenye umri wa miaka 62, amemuua mkewe aliyemzidi miaka miwili kwa kile alichowaambia Polisi wa Katavi kuwa anahisi mwenza wake alikuwa akimloga.
Mwanamke huyo aitwae Farazia
Nzigiyimana, Mhutu mwenye umri wa miaka 60 ambae alikua Mkulima wa Kijiji cha
Kabanga, Kabungu, Wilayani Tanganyika anadaiwa kuuawa na mumewe Nestory
Ntibigimana (62) usiku wakiwa wamelala.
"Ilikua saa tisa usiku,
mwanaume huyo alimuua mke wake kwa kumpiga na kitu chenye ncha butu kichwani na
sehemu ya paji la uso, Mume wake pia ni Mhutu, baada ya tukio mtuhumiwa
alitoroka lakini akakamatwa, tulipomuhoji akasema alifanya hivyo kwa sababu
alikua anahisi Marehemu amekua akimloga," alisema RPC Benjamin Kuzaga.

Post a Comment