WAKANDARASI ACHENI UBINAFSI UNGANENI TUWAPE KAZI- WAITARA
Baadhi ya wajumbe walioshiriki
katika Mkutano wa Mashauriano na wadau wa sekta ya ujenzi wakifuatilia mjadala katika
mkutano huo wa pili ulioandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wakandarasi nchini (CRB)
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara amewataka wakandarasi nchini kuungana na kuacha chuki, ubinafsi na fitna ili wanufaike na miradi mingi ya ujenzi inayotekelezwa na Serikali.
Amesema hayo jana jijini
Arusha wakati akifungua mkutano wa pili wa mashauriano wa wadau wa sekta ya ujenzi
kwa mwaka 2021 ulioandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB), na kusisitiza
nia ya serikali kufanya kazi na wakandarasi walioungana, waadilifu na wenye gharama nafuu.
“Miradi mingi mikubwa
ya Serikal iinafanywa na wakandarasi wageni kutokana na wakandarasi wazawa kushindwa
kuungana na kuitekeleza kwa ubora na kwa muda unaotakiwa”, amesema.
Serikali imejipanga
kutoa kipaumbele kwa wakandarasi wazawa
watakaojiunga ili kuwajengea
uwezo wa kimtaji na kuwawezesha kumudu kujenga miradi mikubwa na hivyo kubakisha
fedha nyingi za miradi hiyo hapa nchini.
“Mkipewa miradi wekeni
gharama nafuu na ikamilisheni kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa ili kujenga imani
kwa Serikali na wananchi kuwa wakandarasi wa ndani wanaweza”, amesisitiza Waitara.
Amewataka wakandarasi
kupambana na rushwa katika miradi na pale wanapoungana kuwa na nidhamu ya ushirika
ili kuwezesha miradi wanayopata kukamilika kwa wakati, ubora na kwa gharama nafuu.
Naibu Waziri Waitara
amewataka wadau wa ujenzi kufanya tathmini kuhusu gharama za ujenzi nchini ili kuja
na bei nafuu itakayowezesha miradi mingi ya Serikali kufanywa na wakandarasi wazawa
na hivyo kuongeza fursa za ajira na kukuza uchumi.
Naye Mwenyekiti wa CRB, Mha. Consolatha Ngimbwa ameiomba Serikali kutumia
wakandarasi waliosajiliwa ili kuwezesha ujenzi nchini kuwa wa viwango vya juu na
kutoa fursa za ajira kwa watu wengi.“
Hali ya wakandarasi
nchini ni mbaya kutokana na matumizi ya force account kwenye miradi mingi ya serikali
na hivyo kuwafanya wakandarasi wengi kukosa kazi amesema Mha. Ngimbwa.
Amesema CRB imewafundisha
wakandarasi wake namna bora ya kutayarisha zabuni na kusimamia miradi ya ujenzi
ili ikamilike kwa wakati.
“Wakandarasi tuko tayari
tunaomba tupewe tujenge mji wa serikali na tulipwe kwa wakati”,amesisitiza Mha.Ngimbwa.
Naye msajili wa wakandarasi
nchini Bw, Reuben Nkori ameiomba serikali iweke vituo vya kukodisha mitambo ili
kuwawezesha wakandarasi kupata vifaa kwa urahisi, ipambane na rushwa katika usimamizi
wa miradi na kuwalipa wakandarasi kwa wakati ili kuwezesha miradi kuwa nafuu.
Mkutano huo wa siku
mbili wa mashauriano unaoongozwa na kauli mbiu “ juhudi za makusudi za wadau kuwezesha
ukuaji wa wakandarasi wa ndani”, pamojan a mambo mengine utajadili na kutoka na
ufumbuzi wa namna bora ya kuwezesha wakandarasi wazawa na sekta ya ujenzi nchini
kukua.
Takriban wakandarasi
11,600 wamesajiliwa nchini na kati yao asilimia 3.5 ni wa kutoka nje na 96.5 ni
wazawa ambao wako tayari kufanya kazi kwa ubora unaozingatia thamani ya fedha.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI MEI 5,2021.

Post a Comment