WAFUKUA MAITI, WANYOFOA VIUNGO MOROGORO

HAKIKA ni nyakati za mwisho. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, watu wenye malengo yasiyofahamika, wamefukua kaburi na kuitoa nje maiti iliyokuwa imezikwa, kisha wakakata viungo vya marehemu na kuondoka navyo, ikiwemo kichwa, figo na sehemu za siri.
Kufuatia unyama huo, watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma hizo zilizofanywa dhidi ya marehemu Rehema Michel.
Kamanda wa Polisi, Fotunatus Musilimu amesema Mwanamke huyo (35)
alipata ajali na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro kwa siku
chake baadaye alifariki.
-
Mwili ulikutwa umekatwa baadhi ya viungo ambavyo ni Kichwa,
Shingo, Sehemu za Siri, Mkono na Mguu wa kushoto na kisha kuupasua Mwili na
kuchukua Pafu la kushoto na Moyo.

Post a Comment