KIWANDA CHA MIKATE CHAOMBA RADHI MTEJA KUKUTA TUNDU KATIKATI YA MKATE, KUMLIPA FIDIA


1.jpg

KIWANDA kimoja nchini Kenya kilicho maarufu sana kwa uokaji mikate kiitwacho Super Loaf, kimemuomba radhi mmoja wa wateja wake aitwaye Kelly Inyani aliyelalamika kukuta uwazi katikati ya mkate alionunua, jambo alilolitafsiri kama kupunjwa mkate ikilinganishwa na thamani ya fedha alizolipa.

Kiwanda hicho kimesema kimepokea kwa huzuni lalamiko hilo na kuahidi kuwa kitamlipa fidia mteja wake huyo pamoja na kumuomba radhi kwa usumbufu alioupata. Hata hivyo haijajulikana ni kiasi gani atalipwa.

No comments