WABONGO BWANA, ETI MARA HII BIASHARA AFADHALI KIDOGO!

HALI ya kibiashara kusema za ukweli ilikuwa ni mbaya, hasa baada ya serikali ya awamu ya tano kuamua kufanya biashara na taasisi zake na fedha zake zote kuhifadhiwa katika akaunti moja Benki Kuu.
Wafanyabiashara
binafsi walikosa tenda katika miradi ya serikali na taasisi zake, fedha
zikapotea mitaani na wengi wakafunga biashara zao.
Lakini miezi
michache tangu kutokea kwa kifo cha Rais wa Awamu ya Tano, John Pombe Magufuli,
wengi wameelezea matumaini ya hali kufunguka, huku baadhi wakikiri kuwa sasa
hivi kidogo afadhali, biashara si kama mwanzo.
Rais Magufuli
alitangazwa kufariki Machi 17 mwaka huu kwa matatizo ya moyo yaliyomsumbua kwa
kipindi cha miaka kumi.

Post a Comment