RC MAKALA ATAKA MAJAMBAZI DAR WAPEWE SHOW KALI


Majambazi Dar wauona moto wa RPC mpya | Dar24

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala amewataka Polisi kuhakikisha wanafanya kila wawezalo ili waweze kudhibiti wimbi jipya la ujambazi lililoibuka kutoka kusikojulikana.

Akizungumza jijini hapo jana, Makala ambaye alipata kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya, moja ya mikoa korofi kwa uhalifu, alisema majambazi hao wamekuja na moto, hivyo dawa ya moto ni moto.

"Nataka Polisi wawape show kali hawa majambazi, wanyang'anywe silaha kabla hawajazitumia," alisema.

Kwa zaidi ya miaka mitano, uhalifu ulionekana kutoweka hasa jijini Dar es Salaam na sehemu kubwa ya nchi, lakini mara tu baada ya kifo cha Rais John Joseph Magufuli, hali inaonekana kubadilika ghafla, kitendo kilichomfanya Rais Samia Suluhu Hassan kukisema hadharani, akimtaka IGP Simon Sirro kuchukua hatua.

No comments