MWANAMKE ALIWAGOMBANISHA CHEGE NA NATURE


Nisifieni kabla sijafa - Said Fella | East Africa Television

 IMEVUJA. Aliyewahi kuwa kiongozi wa kundi la T.M.K Wanaume Family, Said Fella maarufu kama Mkubwa, ametoboa siri kuwa ugomvi kati ya nyota wa kundi hilo, Juma Kassim 'Nature' na Said Chigunda 'Chege' ulisababishwa na mwanamke.

Fella ambaye hivi sasa ni mmoja wa mameneja wa Diamond Platnum katika kampuni ya WCB, alisema awali mwanamke huyo alikuwa ni mali ya 'mtoto wa Mama Said', lakini baadaye akageuka na kumtaka Nature, ambaye enzi hizo alikuwa msanii mkubwa kuliko Chege.

Mwanzoni mwa miaka ya 2010, Nature alijiondoa katika kundi la TMK Wanaume Family na kuanzisha TMK Wanaume Halisi akiwa pamoja na swahiba wake wa tangu utotoni, Haruna Kahena 'Inspekta'.

 

No comments