VIGOGO WIZARA YA FEDHA WAPIGWA CHINI KUPISHA UCHUNGUZI


Kassim Majaliwa: Mfahamu waziri mkuu wa Tanzania - BBC News Swahili

MIEZI takribani miwili ikiwa imepita tangu Rais Samia Suluhu Hassan atoe agizo la kutaka Takukuru kufanya uchunguzi kuhusu fedha zote zilizotolewa Benki Kuu ya Tanzania kati ya Januari na Machi mwaka huu, vigogo kadhaa wamesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa ukwapuaji wa mamilioni ya pesa katika Wizara ya Fedha.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Mkaguzi Mkuu, Mkaguzi Msaidizi na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Fedha. Amefanya hivyo ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya Fedha za Umma.

Wakati akimuagiza Mkurugenzi wa Takukuru ACP Salum Hamduni kufuatilia jambo hilo, Waziri Mkuu alisema fedha hizo zimetolewa kiutata, zikitajwa kuwa ni malipo kwa kazi maalum ambazo hazikutajwa, malipo kwa kazi ambazo ni majukumu ya kila siku ya watumishi hao, malipo ya siku ya Mei Mosi na kadhalika.

Taarifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu iliyotolewa leo Mei 28, 2021 inaeleza kuwa katika kikao kazi na Waziri wa Fedha na Mipango, Katibu Mkuu, manaibu katibu wakuu na watendaji waandamizi wa wizara hiyo mkoani Dodoma jana, Majaliwa amemuagiza mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru), Salum Hamdun kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na ikithibitika si za kweli wahusika warejeshwe kazini.


No comments