CHATO YAKATALIWA KUPEWA HADHI YA MKOA


Madiwani Geita waibana GGM | Habariclouds

IKIWA imepita miezi miwili tangu wazee wa Chato kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan kufikiria kuipa Chato hadhi ya Mkoa, Baraza la Madiwani Geita limeukataa mpango huo na kuupinga kikaoni.

Rais Samia wakati akijibu ombi hilo katika hafla ya mazishi ya Rais John Magufuli iliyofanyika Chato, alisema atalifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuona kama vigezo vya kutangazwa kuwa mkoa vinakidhiwa.

Baraza Maalum la Madiwani Halmashauri ya Wilayani Geita Mkoa wa Geita wamepinga wilaya mpya ya Busanda pamoja na hifadi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo kuchukuliwa na mkoa mpya wa Chato unaotarajiwa kuanzishwa wakidai kuwa itasababisha wananchi kusafiri umbali wa kilomita 200 kwenda kutafuta huduma na kusababisha mkoa wa Geita kukosa sifa kiutawala.

Madiwani hao wamesema baadhi ya maeneo yanayotakiwa kuchukuliwa ili kwenda kujiunga na Chato kupata hadhi ya mkoa, kitaondoa sifa za Geita kuwa Mkoa, jambo ambalo likifanyika halitakuwa na maana.

 

No comments