USHIRIKINA WATAJWA KARIAKOO DERBY

 Yanga close in on Azam as Simba SC suffer first defeat - The Citizen

BAADA ya tambo nyingi za kila namna kutoka kwa wababe wa soka la Tanzania, Yanga na Simba zinazotoka eneo moja la Kariakoo, jijini Dar es Salaam, hatimaye, kwa jinsi isivyotarajiwa, halikupigwa pale Uwanja wa Benjamin Mkapa, kama ilivyopangwa Mei 8, 2021.

Awali, mchezo huo ilikuwa upigwe saa 11 jioni. Mashabiki kutoka kila pembe ya nchi na jirani walijitokeza uwanjani kuanzia majira ya asubuhi hadi mchana wa saa nane, liliposikika tangazo, sambamba na kwenye page za klabu zote mbili kuwa mchezo huo umesogezwa mbele hadi saa moja usiku.

Klabu zote mbili zilithibitisha kupata taarifa hizo za kusogezwa mbele kwa muda. Katika taarifa rasmi ya Shirikisho la soka Tanzania TFF, zilisema suala hilo limetokana na wao kupokea maelekezo kutoka Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa.

Yes, kikanuni, TFF ipo chini ya Wizara hii. Wakati Simba ilikubaliana na jambo hilo la kusogezwa mbele kwa muda, wapinzani wao, walikataa. Yanga walisema watapeleka timu yao uwanjani kwa saa za awali, kwani taarifa ya kusogezwa kwa muda, lilifanyika nje ya matakwa ya kanuni.

Kwamba, ili mechi iweze kusogezwa mbele ya muda wa awali, taarifa inapaswa kutolewa kwa klabu husika, angalau si chini ya saa 24 kabla ya muda wa awali. Kwa kanuni hii, Yanga walikuwa sahihi.

Kwa kuzingatia hilo, Yanga iliwasili uwanjani kwa muda wa awali na baada ya kufanya taratibu zote ingawa hakukuwa na mwamuzi, ilipotimia saa 11.30, baada ya kusubiri kwa dakika 15 ili wapinzani wao watokee, wakaondoka kabisa uwanjani kurejea kambini kwao.

Simba waliwasili uwanjani kwa muda wa mabadiliko, lakini wakiwa uwanjani wakipasha, walisikia tangazo lililosema kuwa mchezo huo umeahirishwa hadi itakapotangazwa tena. Kama ilivyokuwa kwa Yanga, Simba nao wakapanda gari lao na kurejea kambini kwao.

KIMBEMBE KINAANZIA HAPO.....NANI ANAHUSIKA?

TFF kupitia kwa Rais wake, Wallace Karia, anadai wao walipokea maagizo kutoka wizarani kuwa mchezo huo usogezwe mbele kwa vile isingewezekana kuwa na matukio mawili ya kitaifa kwa wakati mmoja.

Ikumbukwe kuwa wakati mchezo huo ukienda kuanza saa 11 jioni, siku hiyohiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alikuwa mgeni rasmi katika shughuli ya uzinduzi wa kitabu cha Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi, shughuli ambayo pia ilihudhuriwa na Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete.

Hata hivyo, TFF ilisema Bodi ya Ligi, ambayo ndiyo msimamizi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ndiyo itatoa taarifa rasmi.

Baadaye, Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, aliitaka wizara na taasisi zinazohusika na sakata hilo, kutoa ufafanuzi wa haraka, ikiwa ni pamoja na namna gani walionunua tiketi watakavyorudishiwa fedha zao.

 

Kufuatia kauli hiyo ya Waziri Mkuu, Bodi ya Ligi imetoa taarifa ambayo hata hivyo, haina tofauti za mwanzo ambazo zimekuwa zikitolewa, huku ikishindwa kutaja ni nani hasa na sababu zipi, zilizosababisha fedheha hiyo kwa familia ya soka nchini.

Wakati sakata hilo likiwa bado limewachanganya mashabiki wa soka nchini, ambao wanasubiri kujua mtu hasa aliyetoa amri ya kusogezwa kwa mchezo huo na sababu zake, maneno yamekuwa mengi baina ya watani hao wa jadi.

Shabiki mmoja kutoka Bagamoyo, ambaye hakutaka jina lake kutajwa, lakini akisisitiza yeye ni mtu wa ndani wa mojawapo ya klabu hizo anaibuka na simulizi hii...

"Unasikia bwana, jamaa zetu walikuwa wanajua kabisa kuwa game hii inaenda kula kwao, kwa hiyo walijaribu kila mbinu, lakini kila wakirudi mezani, ubao ulikuwa unasomeka kwa wao kupoteza.

"Mara ya mwisho kuchungulia, wakakuta wanapigwa WIKI. Ikawa hamna namna. Ndipo mwenzao mmoja, akaja na wazo la kumtumia mtu wa nje yao ili aharibu mambo. Ndiyo akapendekeza MTU AHARIBIWE AKILI AHARIBU MCHEZO.

"Ndipo huyo jamaa, bila kujifahamu, kwa nafasi yake, akajikuta akiinua simu na kuwapigia TFF akitaka mchezo huo usogezwe mbele. Tunasikia baada ya hao wenzetu kupata ile taarifa ya kuahirisha mechi, walirukaruka kwa furaha wakijua mipango yao imekubali.

"Ndipo sasa wakawa wamepata pa kutokea. Waliposikia na sisi tumekubali mabadiliko ya muda, wakazidi kushangilia kwani hilo ndilo hasa walilolitaka. Ndiyo maana wakakomalia kuvunjwa kwa kanuni na hivyo kuepuka kipigo.".....

Shabiki mwingine yeye anadai ukweli ni kwamba timu zote mbili zingeweza kushuka dimbani na kuucheza mchezo huo, lakini kitu ambacho watu walikuwa hawajui ni kuwa kila aliyetaka muda wake alifaidika na matokeo.

"Mechi ile kama ingepigwa ule muda wa awali, Simba alikuwa anatota, tena kwa bao nyingi, ndiyo maana nin kama Mnyama alifurahi sana kubadilishwa kwa muda, kwani wazee wa milingotini wanasema, kwa mchezo ule kupigwa usiku, Wekundu walikuwa wanashinda.

"Sasa ndiyo maana unaona Yanga ambayo ilikuwa ishinde mchana, ikakataa kucheza usiku na Simba ikafurahia mchezo huo kuahirishwa muda wa awali.

UKIACHANA na imani hizo za kishirikina, mchawi wa mchezo huo ni TFF na Bodi ya Ligi. Period!

 

 

No comments