UKIONA MWANAMKE WAKO AMEACHA KULALAMIKA KUHUSU MAMBO ULIYOKUWA UNAMFANYIA JUA KUNA:

FANYA ujinga wako unavyoweza,
lakini ukiona mwanamke ameacha kulalamikia mambo ambayo zamani ilikuwa ni
kelele kubwa kati yenu basi jua kuwa kuna mambo yafuatayo.
1) Jambo la kwanza inawezekana
kuwa kashaanza kukuchoka na hajali tena.
2) Jambo la pili inawezekana ana
mtu mwingine ambaye anampa amani, hata kama huyo mtu anajua hawawezi kuwa
pamoja lakini angalau ana furaha kidogo na huyo mtu kuliko akiwa na wewe mume
wake wa ndoa.
3) Jambo la tatu ni kwamba huyo
mwanamke kashakukatia tamaa kuwa hutabadilika na kaamua kujipa furaha yake
mwenyewe.
4) Jambo la nne wengi wakiona
wanawake zao wapo busy na mambo yao udhani wana mwanaume mwingine sio kweli,
mwanamke akichukia anachukia kweli kweli. Unakuta wala hachepuki, na wala hana
mpango wa kukuacha, wala hana mpango wa kutafuta mtu mwingine.
5) Jambo la tano usiombe mkeo au
mpenzi akae ajiulize mambo haya:
1} Hivi nahangaika nini?
2} Nitapiga kelele mpaka lini?
3} Nitajibiwa matusi mpaka lini?
4} Nitahangaika na wanawake zake
katika mitandao mpaka lini?
5} Hivi mimi ni mtu gani kila
siku kupekua simu yake na kukuta mapicha ya uchi?
6} Hivi huyu mwanaume ni pumzi
kwamba nisipohangaika naye nitakufa?
Hayo ni maswali mabaya sana
mwanamke akijiuliza, sasa ole wako apate jibu.
Kwa, hiyo naomba utambue kuwa
ameacha kuhangaika na wewe na ameamua kujihangaikia. Ameamua kupendeza kwa
ajili yake, ameamua kudili na maisha yake, kujifurahisha bila kujali kama
umenuna au unaendelea na upuuzi wako!
Mwanamke akishachagua kuwa na
furaha yake mwenyewe basi jua kuwa ni zamu yako ya kuteseka, ni zamu yako ya
kukagua simu yake, ni zamu yako ya kupiga simu na kutuma meseji miamia kuulizia
kuwa yuko wapi?
USHAURI WANGU:
Kama una mwanamke ambaye anakupenda sasa hivi, angalau anakuuliza kwanini unarudi saa nane basi mpende, mpe hata jibu zuri hata kama ni la uongo lakini acha kumtukana na kumdhalilisha.
Siku akijiuliza yale maswali 6,
Mimi nitamsaidia kumpa jibu, hapo ndio utajua kuwa jela ya mapenzi ni mbaya
kuliko hata Keko na Segerea.
MUNGU akubariki sana.
EV Daniel Nzelani
0763100472

Post a Comment