TUMTUMIE DIAMOND KUTOBOA -PRODYUSA S2KIZZY

SALMIN Kassim Maengo ambaye anafahamika zaidi kisanii kama s2kizzy amewataka watayarishaji wenzake wa muziki wa Bongo Flava, kumtumia nyota mkubwa Diamond Platnum katika kufikisha uwezo wao kimataifa, kwani ndiyo levo wanazozitafuta.
Prodyusa huyo ndiye
anayefanya kazi ya kuandaa albamu mpya ya msanii huyo mwekezaji, ambayo
inatakwa kuwashirikisha wasanii wakubwa kutoka kila pembe ya dunia. Na katika
kuhakikisha kazi hiyo inafanyika katika viwango, S2kizzy amewaalika maprodyusa
wengine nchini kujumuika naye kuingiza sound zao.
Kupitia The Switch,
mtayarishaji huyo ambaye pia anafahamika kama Zombie alisema; ''Kwanza
nashukuru kwakKuwa kwenye album ya Diamond, unaposhiriki kwenye album kubwa kama
hii hata kama umefanya wimbo mmoja ni kitu kikubwa na unajifunza vitu vingi kwa
sababu inahusisha kolabo kubwa na mipango mikubwa.
"Mimi napenda kuwapa
nafasi Producers wenzangu haswa wachanga, napenda wafike sehemu kubwa so as
long as tuna sound nyingi na watu hulalamika tunashindwa kuwafikia wasanii wakubwa;
'So mimi natoa
nafasi na kupitia mimi producers wengine wanaweza wakapata nafasi ya kufanya
naye kazi (Diamond) huenda nyimbo zao zikasikika mwisho wa siku wote tunataka
muziki wetu ufike mbali zaidi, naweza nikawa kitu sina mimi, akawa macho
Mwingine, hivyo album ikiwa na sound nyingi na tofauti ndio itafanya muziki
wetu uwe mkubwa zaidi.
"Diamond ni
msanii mkubwa sana na msanii wa kimataifa ni moja kati ya icon ambazo tunazo kwa
hiyo mtu ambaye anatuwakilisha vizuri nje, ni vyema tukamtumia yeye mwenyewe
kufikisha muziki wetu mbali kwa upande wa producers''.
S2kizzy ni
mtayarishaji ambaye ameshafanya kazi kadhaa zilizomshirikisha Diamond kama
Tetema aliyofanya na Rannyvan, pia amefanya kazi na wasanii wengi wakiwemo Jux,
Vanessa Mdee, Rannyvan, Harmonize, Whozu na wengine kibao.

Post a Comment