RAIS SAMIA ASUBIRIWA KWA HAMU NEEMA MEI MOSI LEO

LEO ni siku ya
maadhimisho ya wafanyakazi duniani kote na kitaifa, sherehe hizo zinafanyika
jijini Mwanza ambako mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Samia Suluhu Hassan.
Maelfu ya
wafanyakazi kote nchini, leo watakuwa wakimsubiri rais huyo wa kwanza mwanamke
nchini, kutamka kile ambacho hawajawahi kukisikia kwa takribani miaka sita
iliyopita, nacho ni nyongeza ya mishahara na upandaji madaraja.
Watumishi wa umma
wameshindwa kupandishiwa mishahara na madaraja yao kwa kipindi chote cha
serikali ya awamu ya Tano, iliyokuwa chini ya hayati Rais John Pombe Joseph
Magufuli.

Post a Comment