TUMEPEWA AKILI ZA KUFIKIRI, SI KUTISHANA- RC MTAKA
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Antony
Mtaka akiwa katika vikao vya kuanisha vipaumbele mkoani , amesema yeye hayupo
pale kutisha na kumtishia mtu bali yupo pale kwa ajili ya kuunganisha akili za
watu waliozajaliwa ili kuleta matokeo mazuri mkoani humo.
RC Mtaka, amesema watumishi wa wilaya zote Dodoma wachague
vipaumbele vichache, hawana haja ya kuwa na vipaumbele vingi.
Akitolea mfano kwa wilaya ya Kongwa kwa Job Ndugai,
Mheshimiwa Mtaka amesema Kongwa kuna ng'ombe wengi sana, lakini Je kipaumbele
kiwe nyama au maziwa au uzalishaji wa ng'ombe zaidi?
Amesisitiza kwa wilaya ya Kongwa hakuna haja ya kushika vipaumbele
vyote kwa wakati mmoja, ni kuchagua kimoja na kuunganisha akili na mawazo ili
kupata manufaa.
RC Mtaka amesisitiza vipaumbele vikiwa vingi sana vinatutoa
kwenye mstari na baadae tunapata matokeo mabaya
RC Mtaka amesisitiza anapenda astaafu kazi kwa heshima na
hata watu wakimuona waweze kumsalimia na kucheka pamoja, Amesisitiza watu
inabidi waone fahari kuwaona viongozi wao Dodoma.
Aidha maeneo ambayo wanalima alizeti RC Mtaka amesema suala
sio kulima alizeti tu, suala ni kujua katika alizeti kipaumbele ni mafuta au
alizeti yenyewe?
RC Mtaka ameeleza kuwa ni muhimu kuzalisha kwa kuangalia soko
lipo wapi? Ni soko la ndani au la nje, na Je kuna uhitaji wa hilo zao sokoni.
RC Mtaka amesisitiza kuwa RC Mahenge anayeondoka Dodoma
alikuwa mtu mpole na mnyenyekevu sana na hakuwa na walinzi kwenye mambo yake
nje ya ofisi kwani aliishi maisha ya kuheshimu watu.
RC Mtaka amesisitiza anapenda siku akifikisha umri wa RC
Mahenge na yeye awe mtu humble na mcheshi sana.
Akihoji kama RC Mahenge alikuwa anatembea bila ulinzi,
kwanini Mkuu wa wilaya ujaze walinzi?

Post a Comment