TRIPPLE C ATOA NENO KWA KAIZER CHIEFS


Inaweza kuwa picha ya mtu mmoja au zaidi, watu wanacheza kandakanda na nyasi

KIUNGO na staa namba moja wa Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba, Clatus Chota Chama raia wa Zambia, amekiri kushindwa kwa timu yake na kuwatakia kila la kheri wapinzani wao Kaizer Chiefs.

Mfungaji huyo wa bao la tatu katika mchezo wa marudiano, amesema licha ya kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika anajivunia timu yake ya Simba kwa mapambano iliyofikia.

Amesisitiza kuwa hawajakata tamaa katika michuano hiyo hadi wafanikiwe kupata kile wanachokihitaji hivyo wanajipanga kwa ajili ya msimu ujao.

"Safari yetu ya Ligi ya Mabingwa imeisha, najivunia timu yangu kwa sababu kila mchezaji ameonyesha kiwango cha hali ya juu lakini haikutosha.

"Hatutaacha mpaka pale tutakapofanikiwa, tuonane kipindi kijacho nawatakia kila la kheri Kaizer Chiefs katika hatua yao ya Nusu Fainali." alisema Chama.

 

No comments