NAHODHA SIMBA ALAMBA MILIONI MBILI UNUSU

NAHODHA wa timu ya soka ya Simba, John Raphael Boko maarufu kama Adebayor, amezawadiwa kitita cha shilingi milioni mbili na nusu kama zawadi baada ya kuibuka kuwa mchezaji nyota wa mechi baina ya timu yake dhidi ya Kaizer Chiefs.
Boko ambaye ametumia muda mwingi akiwa nje kutokana na majeruhi, alicheza mechi hiyo tangu mwanzo, akifunga mabao mawili katika ushindi wa Simba wa mabao 3-0 ambao hata hivyo, ulihitimisha safari ya timu hiyo hatua ya roboi fainali.
Kitita hicho kilitolewa na kampuni
ya Emirates Alminium ambao wana mkataba na Simba wa kuwazawadia wachezaji wao
wanaoibuka bora katika kila mechi kwa kila mwezi.

Post a Comment