ARIEL SHARON, WAZIRI MKUU ISRAEL ALIYEZIMIA KWA MIAKA 8

KUNA
watu wana historia zenye kutatanisha sana hapa duniani. Miongoni mwao ni
aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa taifa la Israel, Ariel Sharon.
Alipokuwa mwanajeshi, alijulikana kwa ushujaa
wake katika uwanja wa mapambano kwa miongo kadhaa kufuatia kuundwa kwa taifa la
Israel, akijulikana hasa wakati wa vita vya Jom Kippur vya mwaka 1973. Katika
mbinu za hali ya juu alizozionyesha, aliwaongoza wanajeshi wa Israel kuvuka
mfereji wa Suez na kulikabili jeshi la Misri.
Pia alijulikana na wengi kwa kuwa jabari na
mbabe. Mwaka 1982, aliongoza uvamizi wa Lebanon ambao ulipelekea mauaji
yaliyofanywa na wanamgambo wa Lebanon kwa mamia ya Wapalestina katika kambi za
wakimbizi za Sabra na Shatilla huko Beirut.
Kama mwanasiasa, Ariel Sharon pia alikuwa na
utatanishi. Akiwa waziri, alihamasisha kuundwa kwa makazi ya walowezi wa
Kiyahudi kote katika maeneo ya wapalestina.
Serikali yake ilizikandamiza vurugu katika
muda wa miaka michache, na kuanza kazi ya kuweka vizuizi vya usalama ambavyo
hivi sasa vinawatenga waisraeli na wapalestina.
Mwaka 2006, bwana Sharon alipata mfululizo wa
matatizo ya kiharusi na kuingia katika hali ya kupoteza fahamu iliyopelekea
kuwa kwenye COMA kwa miaka nane toka 2006 Hadi 2014 alipofariki. Nafasi yake ya
waziri mkuu ilichukuliwa na Ehud Olmert.
Wasifu wa Ariel Sharon, Mtu asiyejali
Ariel Sharon alikuwa mtu asiyejali,mwenye aina
ya ukaidi, asiyejali nani anayempenda wala anayemchukia iwe ni Waisrael au
Waarabu.
Malengo ya kwanza ya mwanajeshi huyu mstaafu
na veterani wa siasa ilikuwa ni kuhakikisha kwanza usalama wa Israel kwa vile
alivyoamini.
Sharon hakujali chochote kwa wale wasioamini.
Ndio maana alihakikisha ardhi kubwa na haki ya
kisiasa inasalia kwa Waisrael na kutoa nafasi ndogo kwa Wapelestina.
Bwana Sharon alizaliwa nchini Palestina mwaka
1928, ilipokuwa chini ya utawala wa Kiingereza.
Akiwa kijana mdogo alijiunga na kitengo cha
jeshi la chini kwa chini la Wayahudi la Haganah na kupigana katika vita vya
Israel na Waarabu mwaka 1948-49 baada ya kuundwa kwa taifa la Wayahudi.
Kwenye miaka ya 1950 aliongoza oparesheni kali
ya kijeshi dhidi ya kituo cha jeshi la Misri kilichopo kwenye ukanda wa Gaza, katika
tukio moja la mwaka 1955 wanajeshi wa misri 38 waliuwawa.
Bwana Sharon alipanda kicheo kutoka brigedia
hadi jenerali na kamanda wa kikosi cha jeshi kwenye vita vya siku sita vya
mwezi Juni mwaka 1967 ambapo Israel iliuteka ukanda wa Mashariki wa mji wa
Jerusalem, Ukindo wa Magharibi na ukanda wa Gaza.
Uny'ang'anyi huo wa nguvu uliofanywa na jeshi
la Wayahudi ilizidisha chuki ya Wapalestina kwa mtu ambaye alikuwa adui yao
mkubwa.
Ariel Sharon
Alichaguliwa kwa mara ya kwanza kwenye bunge
la Israel lijulikanalo kama Knesset mwaka 1973, lakini akajiuzulu mwaka mmoja
baadaye ili kutumikia nafasi kama mshauri wa usalama wa aliyekuwa waziri mkuu
wa tano wa taifa la Israel bwana Yitzhak Rabin.
Alichaguliwa tena kwenye bunge la Israel mwaka
1977.
Bwana Sharon alikuwa kinara wa uvamizi wa
Israel nchini Lebanon mwaka 1982.
Akiwa kama waziri wa ulinzi na bila kumueleza
Waziri Mkuu Menachem Begin alituma vikosi vya jeshi la Israel kwenda mjini
Beirut, uvamizi ambao ulimaliza na kufukuza chama cha ukombozi cha Palestina
kilichokuwa kikiongozwa na Yasser Arafat cha Palestine Liberation Organisation
(PLO) kutoka nchini Lebanon.
Uvamizi huo ulisimamisha mashambulizi
yaliyokuwa yakifanywa na PLO kupitia nchini Lebanon kuipiga Israel na pia
ilisababisha uteswaji mkubwa wa mamia ya Wapelestina kutoka kwa wapiganaji
wakristo kutoka Lebanon chini ya amri ya wanajeshi wa kiyahudi kwenye kambi ya
wakimbizi.
Bwana Sharon aliondolewa madarakani mwaka 1983
na mahakama ya Israel ya uchunguzi ya uvamizi wa mwaka 1982 nchini Lebanon,
ambapo ilimkuta na makosa kutohusika moja kwa moja na mauaji.
Kwa wanasiasa wengi na wale waliokuwa na
mtazamo kama wake huo ndio ulikuwa mwisho wake wa kisiasa.
Lakini kwa bwana Sharon alisalia kiongozi
maarufu wa Wayahudi wenye mrengo wa kulia na kuwa imani kwamba muda ungalipo na
nafasi nyingine itajitokeza tu.
Ariel Sharon malengo yake ambayo maadui zake
waliyaita ya hatari na yenye kukandamiza, ilikuwa ni kupigania hali ya usalama
wa ulinzi wa Israel, aliamini daima kwamba mwisho hilo lingekuwa suluhisho la
haki.
Akiwa waziri wa nyumba kwenye miaka ya 1990, alisimamia
na kuongoza ujenzi mkubwa majengo ya wayahudi kwenye Ukingo wa Magharibi na
Ukanda wa Gaza tangu Israel iyachukue maeneo hayo kwenye vita vya siku sita.
Baada ya Chama chenye mrengo wa kulia cha
Benjamini Netanyahu kuchukua madaraka mwaka 1996, Waziri mkuu mpya wa Israel
alitia chagizo kumweka jenerali huyo wa zamani wa jeshi kwenye baraza lake la
mawaziri.
Wakati alipomchagua kama Waziri wa mambo ya
nje mwaka 1998, Bwana Netanyahu alisema Ariel Sharon alikuwa mtu sahihi kwa
nafasi hiyo.
" Hatutakiwi kufikiria yaliyopita"
alisema. " ana rekodi katika maisha yake yote ya kutumikia umma na katika
miaka 15 iliyopita watu wanatakiwa kujivunia naye."
Bwana Sharon alichaguliwa kuwa kiongozi wa
chama wa mrengo wa kulia cha Likud kilichokuja kuwa chama cha Upinzani baada ya
anguko kubwa la Netanyahu kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 1999.
Baada ya kushindikana kwa mapatano kwenye
mkutano wa amani ya Palestina na Israel ujulikanao kama Camp David mwaka 2001, Sharon
alipigania tena kurejea kwenye ofisi za umma akimpinga waziri mkuu wa wakati
huo Ehud Barak,huku akimtuhumu kwa kuwa tayari kuiuza Jerusalem kwa ajili ya
mapatano ya amani.
" Barak hana haki ya kukata tamaa juu ya
Jerusalem, ambayo watu walipokea kama urithi," Bwana Sharon alisema kwenye
mojawapo ya vikao vya bunge.
Ziara yake yenye utata mwaka 2000 kwenye
msikiti wa Al Aqsa mashariki mwa Jerusalem, eneo ambalo pia ni eneo takatifu
kwa Wayahudi, ilikuwa ni kutonesha kidonda kwa mara ya pili kwa kuamsha
vuguvugu la Wapelestina.
Wasioamini wanasema bwana Sharon alijuwa fika
kuwa ziara yake hiyo ingeleta vurugu na alifanya hivyo kwa makusudi ili
kuwaonyesha Wayahudi kuwa kiongozi kama yeye ndiye atakayeweza kumudu hali
hiyo.
Lakini kwa mara nyingine tena, bwana Sharon
hakuwahi kusikia wala hakujali wasioamini walimweleza nini.
Katika nyakati fulani kwenye mikutano ya
kampeni za uchaguzi mkuu aliwahi kusema anajiandaa kufanya mazungumzo na
kuingia makubaliano ya amani na Waarabu lakini sio chini ya vitisho.
Licha ya yote alikuwa tayari kufanya lolote
ili kuondoa hali ya uonevu utakao ondoa "haki ya Wayahudi kuishi kwa amani
kwenye ardhi yao"
Credit: Jamii Forum

Post a Comment