SIMBA YAOTESHA MAJANI KIBARUA CHA KOCHA KAIZER CHIEFS


POZI LA KOCHA MKUU WA KAIZER CHIEFS LAWA GUMZO

LICHA ya kufuzu kwa Nusu Fainali za Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Klabu ya Kaizer Chiefs imevunja mkataba wa aliyekuwa kocha wake Gavin Hunt. Kocha huyo alijiunga na Kaizer Chiefs September 2020 na kuifundisha timu hiyo katika msimu wa 2020/21.

Baada ya kushinda mechi ya kwanza hatua ya robo fainali kwa mabao 4-0 kule Johannesburg, wawakilishi hao wa Afrika Kusini walipigwa mabao 3-0 na Simba katika mchezo wa marudiano jijini Dar es Salaam.

Hunt akiwa kocha wa Amakhosi aliiongoza timu hiyo kwenye mechi rasmi 44 kwenye mashindano yote. Ameshinda mechi 12, Sare 17, amepoteza 15.

Katika kipindi hiki Makocha wasaidizi Arthur Zwane na Dillon Sheppard wataiongoza timu.

No comments