SIMBA WALAMBA BONASI YA MILIONI 50 TOKA SPOT PESA

WADHAMINI wakuu wa timu ya Simba, kampuni ya Spot Pesa, leo wameikabidhi timu hiyo hundi ya shilingi milioni 50, ikiwa ni bonasi kufuatia kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika Msimu huu.
Tarimba
Abbas, Mbunge wa Kinondoni na Mwakilishi wa kampuni hiyo nchini, alikabidhi
mfano wa hundi hiyo kwa CEO wa mabingwa hao wa nchi, Barbara Gonzalez leo
jijini Dar es Salaam.

Post a Comment