RAIS, WAZIRI MKUU WAVULIWA MADARAKA, WAACHIWA HURU MALI
SIKU tatu baada ya kukamatwa na kuwekwa kizuizini na Jeshi la Nchi ya Mali kwa amri ya Makamu wa Rais, aliyekuwa Rais wa mpito wa taifa hilo la Afrika, Bah Ndaw na Waziri Mkuu, Moctar Ouone wamevuliwa nyadhifa zao na kisha kuachiwa huru.
Kisa cha kukamatwa kwao ni baada ya
kufanya mabadiliko serikalini pasipo kumshirikisha Makamu wa Rais, ambaye ni
mwanajeshi aliyefanya mapinduzi ya Kijeshi yaliyomtoa madarakani Rais Ibrahim Boubakar
Keita miezi tisa iliyopita.
Mzozo wa Kisiasa unalikumba Taifa hilo miezi tisa baada ya
Jeshi kumpindua Keita aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo kuanzia mwaka 2013 hadi
Agosti 2020. Tayari serikali ya Marekani imetangaza vikwazo kwa nchi
hiyo ambayo sasa inaendeshwa kijeshi.

Post a Comment