SIMBA 4G KWA MADIBA
![]()

WAKATI mashabiki na
wapenzi wa soka Tanzania wakiamini mwakilishi wa nchi katika Michuano ya Ligi
ya Mabingwa Afrika, Simba ya Tanzania itaibuka na ushindi katika
mchezo wake wa kwanza wa robo fainali dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika
Kusiini leo, wekundu hao wa Msimbazi, wamechezsea kichapo cha mabao 4-0.
Licha ya kucheza soka
lao safi la kutandaza kandanda uwanjani, mabingwa hao mara tatu wa Ligi Kuu
Tanzania Bara, walikosa mbinu za kuzuia mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya
timu hiyo, inayoshika nafasi ya tisa katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Afrika
Kusinii.
Kwa matokeo hayo, Simba
inatakiwa kuipiga Kaizer Chiefs mabao matano kama inafikiria kuchezo nusu
fainali za Africa's Champions League msimu huu.
Walichekelea sare ya
watani wao Ruangwa, wao wamenuna kwa kipigo 'hevi' kwa Madiba. Hata hivyo,
tofauti na WANANCHI, WEKUNDU WA MSIMBAZI wanaweza kupindua matokeo katika
mchezo wa marudiano. Kumbuka, mwaka 1979, walipigwa 4-0 nyumbani Dar es Salaam
na Mufulila Wonderes ya Zambia, lakini wakaenda kumpiga 5-0 jijini
Lusaka. Katika soka, nothing is impossible.
NB Tunaomba radhi kwa
kusema timu iliyoifunga Simba mwaka 1979 kuwa ni Nkana, ukweli ni kwamba timu
hiyo ni Mufulila Wonderes.

Post a Comment