SASA NI RASMI TANZANIA TIMU NNE CAF MWAKANI
SASA ni rasmi kwamba Tanzania Bara itaingiza timu nne katika Michuano ya Kimataifa msimu ujao baada ya klabu ya ASC Jaraaf ya Senegal kutolewa katika la Shirikisho.
Timu hiyo ya Senegal ilitolewa kwenye mashindano ya kombe la shirikisho na klabu ya Cotton Sports ya Cameron katika hatua ya robo fainali.
Kwa matokeo hayo, Tanzania inabaki na pointi zake 27.5 huku Senegal ambayo ndiyo ilikuwa tishio kwake, kusalia na pointi zake 15.
Pointi hizo za Tanzania
zimetokana na timu zake tatu kufanya vizuri katika michuano ya Afrika ndani ya
miaka mitano iliyopita ambazo ni Yanga iliyochangia pointi 2.5, Namungo pointi
2.5 na Simba iliyochangia 22.5.

Post a Comment