MPOKI ADOKEZA 'WALIVYOPENYA' UGOMVI WA MANJI NA MENGI


Cheka kidogo na JK comedian alivyowaigiza sauti za original comedy - YouTube

MCHEKESHAJI mahiri hapa nchini, Mpoki amedokeza jinsi ugomvi kati ya wafanyabiashara maarufu nchini, marehemu Reginald Abraham Mengi na Yussuf Manji ulivyowapelekea wao 'kutoboa'.

Mpoki pamoja na wenzake Masanja Mkandamizaji, Joti, Mac Reagan chini ya Seki, walikuwa na kundi lao la Comedy, wakirusha vichekesho vyao katika televisheni ya ITV.

Lakini katika kile kilichoonekana kuwa ni masilahi, kundi hilo liliingia katika mzozo na mzee Mengi na hivyo kuwafanya wajiondoe.

“Matajiri wakigombana, maskini anapita katikati...” amesema Mpoki na kueleza kwamba Manji aliwapa mkataba mnono, akawasafirisha kwenda Uingereza. 

Akizungumza katika kipindi cha Joto la Asubuhi kinachorushwa na kituo cha redio cha EFM, Mpoki anasema ugomvi wao na mzee Mengi ulikuwa mkubwa ambao licha ya kushindikana mahakamani, ulimalizwa na aliyekuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Katika hatua nyingine, mchekeshaji huyo ambaye pia ni mtangazaji wa kituo hicho, alisema hapendi kuyaanika maisha yake binafsi, yeye na familia yake.

No comments