RPC DAR AANZA KAZI KWA KISHINDO

KAMANDA wa Polisi
Kanda Maalum y Dar es Salaam, ambaye aliteuliwa hivi karibuni, ameanza kazi kwa
kishindo cha aina yake baada ya kutoa taarifa kuhusu kukamatwa kwa majambazi na
bidhaa kadhaa zilizoibiwa.
Jeshi la Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na Operesheni Maalum ya kupambana na
vitendo vya kihalifu Katika maeneo yote ya Jiji la Dar es Salaam katika dhima
nzima ya Usalama wa Raia na Mali zao na limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 20
na vielelezo mbalimbali kama ifuatavyo:-
1. Majambazi watano
wapora silaha wakamatwa
Mnamo tarehe
18/03/2021 majira ya saa 8.00 usiku majambazi wapatao watano walivamia katika
nyumba ya Mkurugenzi wa Benki ya Azania iliyopo Mbweni Mpiji na kuwashambulia
walinzi wa kampuni ya SUMA JKT na kuwapora silaha aina ya Short Gun Pump Action
ikiwa na risasi tano.
Jeshi la Polisi
Kanda Maalum DSM lilifanya ufuatiliaji na kufanikiwa kukamata silaha hiyo
tarehe 20/05/2021 na watuhumiwa watano waliohusika katika tukio hilo.
2. Watano
washikiliwa kwa mauaji
Jeshi la Polisi
Kanda Maalum ya DSM linawashikilia watu watano kwa tuhuma za mauaji.
Watuhumiwa hao ni:-
1. Issa Karim@
Mdaka Bomu, Miaka 33, Mkazi wa Mbezi
2. Mohamed
Juma@Mabangi, Miaka 31, Mkazi wa Mbezi Mwisho
3. Selemani
Seif@Dullah Kishandu, Miaka 34, Mkazi wa Mbezi Mwisho.
4. Samsoni Joseph
mjeuri, Miaka 32, Mkazi wa Mbezi
5. Ezekiel
Kennedy@Simba MC,Mkazi wa Mbezi
Ambapo, mnamo tarehe 08/05/2021 majira ya 8:05 usiku huko Mikocheni A watuhumiwa hawa walivamia katika bar iitwayo Imbizo Bar na kumshambulia kwa mapanga na marungu mlinzi aliyefahamika kwa jina Regan Sylivester na kusababisha kufariki dunia papo hapo.
Aidha watuhumiwa wanahusika na tukio la unyan’ganyi wa kutumia silaha huko Mabwepande ambapo mnamo tarehe 07/05/2021 majira ya 09:00 usiku walivamia katika kituo cha kuuzia Mafuta (Petrol station) cha MEXONS na kuwashambulia walinzi, wahudumu na wateja na kupora kiasi cha Tsh 2, 440,000/= na kisha kupora silaha aina ya Short Gun ya walinzi hao.
3. Pikipiki, magari manne yaliyoibwa yakamatwa
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limefanikiwa kukamata magari manne na watuhumiwa wanne.
Watuhumiwa hao ni
:-
1. Babuelly Simon
Chao, Miaka 43,Mkazi wa Moshi
2. Sebastiani
Shembaru, Miaka 36, Mkazi wa Kigamboni
3. Hussen Misanya,
Miaka 33, Mkazi Mabibo Relini.
4. Said Rajabu, Miaka 16, Mkazi wa Mabibo
Watuhumiwa hawa
wamekuwa wakiiba magari maeneo ya Kinondoni na Ilala na walikamatwa na magari
yafuatayo:-
1. T 817 ATQ Toyota
Nadia
2. T 134 BPJ Toyota
IST
3. T 952 CKB Toyota
Mark II Grand
4. T 590 DTK Toyota IST
Aidha, Jeshi la
Polisi Kanda Maalum DSM limefanikiwa kukamata Pikipiki namba MC 136 CSA Boxer
nyeusi iliyokwa imeibiwa tarehe 15/05/2021 huko maeneo ya Kibamba shule na
kupelekwa Gairo Mkoani Morogoro.
Jeshi la Polisi Kanda lilifanya ufuatiliaji na kufanikiwa kuikamata pikipiki hiyo na kuirudisha Jijini DSM.
4. Watano
washikiliwa kwa kuvunja na kuiba usiku
Mnamo tarehe 23/05/2021 majira ya saa 08:30 usiku huko Mtaa wa Mikocheni A walivunja nyumba ya Daud Ramadhani na kuiba vitu mbalimbali.
Watuhumiwa wamekamatwa wakiwa na baadhi ya mali walizoiba ikiwa ni pamoja na TV moja aina ya LG NCH 55 Flat screen,Simu mbili aina ya iphon, Laptop mbili aina ya Dell na Mouse nne za kompyuta.
Watuhumiwa hao ni:-
1. Abeid Said@Gebe,
Miaka 41, Mkazi wa Kinondoni
2.Laurent Mwazembe,
Miaka 44, Mkazi wa Malamba Mawili.
3.Ramdhani Mohamed,
Miaka 31, Mkazi wa Mbezi
4.Julias
Mapunda,Miaka 34, Mkazi wa Mbezi Njeteni
5.Emmanuel Zongo,
miaka 30, mkazi wa Kigamboni
5. Sita
washikiliuwa kwa uvunjaji
Jeshi la Polisi
Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia
watu sita (6) kwa
tuhuma za uvunjaji maduka usiku na kuiba.
Watuhumiwa hao ni :-
1. Kaburu Mohamed
kaburu,(30),Mkazi wa Buza Kanisani.
2. Iddi Ally
Kiduku, Miaka 30, Mkazi wa Tandika.
3. Said Ramadhani
@Timu, Miaka 33, Mkazi wa Kitunda.
4. Lucas
Danford@Udongo wa Maka, Miaka 31, Mkazi wa Buguruni
5. Shaban
Bakari@Majani, Miaka 33, Mkazi wa Tandika kaburi moja.
6. Khamis Bahati Chief, Miaka 38, Mkazi wa Buza kwa mama kibonge.
Watuhumiwa hawa wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya uvunjaji maduka nyakati za usiku katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam hususani katika mitaa ya Kariakoo na Ukonga Banana.
ONYO, Jeshi la
Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linatoa onyo kali kwa wahalifu wanaojihusisha
na vitendo vya kihalifu waache mara moja kwani Jeshi lipo imara na limejipanga
vizuri kuhakikisha hali ya Jiji inaendelea kuwa shwari.
Camillius M.Wambura
- SACP
KAMANDA WA POLISI,
KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.
25/05/2021

Post a Comment