MBOWE AONGOZA KIKAO CHADEMA ARUSHA

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Freeman Mbowe leo ameongoza kikao cha Kamati ya Utendaji Kanda ya
Kaskazini kilichofanyika jijini Arusha.
Kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa leo Jumanne tarehe 25 Mei 2021 na Chadema, kupitia ukurasa
wake wa Twitter, chama hicho kina mpango wa kuzindua kile kilichoitwa
Operesheni Haki hapo Alhamisi.
Taarifa ya Chadema
imesema kuwa, lengo la operesheni hiyo ni kudai katiba mpya, tume huru ya
uchaguzi, pamoja na uimarishwaji misingi ya haki nchini.
“Leo Mei 25, 2021,
Mwenyekiti wa chama Taifa, Freeman Mbowe, ameendesha Kikao cha Kamati Tendaji
ya Kanda ya Kaskazini, jijini Arusha,” imesema taarifa ya Chadema.

Post a Comment